Portal talk:Sw
Kutafsiri Jumbe Kiswahili katika BetaWiki!
Lloffiwr, salam. Hali yako ndugu yangu, natumai humzima. Nami pia sijambo! Haya, naona uliacha ujumbe wako katika ukurasa wangu majadiliano katika BetaWiki, ukiwa unazungumzia masuala ya utafsri wa jumbe za MediaWiki. Sidhani kama ni wazo baya kwa upande wangu. Naona ni vyema tu, kwani itarahisisha mambo mengi mno. Kingine nimefurahia kumpata mwenyeji wa Kiingereza! Awali nilikuwa na Wajerumani tu wenye kujua Kiwango cha juu cha Kiingereza, lakini sio lugha yao ya mama! Basi hata nitakuja kukuuliza maswali mawili matatu yahusianayo na Kiingereza, je, utalidhia? Naomba jibu hapahapa latika ukurasa wako wa majadiliano!--Muddyb Blast Producer 13:38, 3 Rhagfyr 2008 (UTC)
- Salam. Mimi sijambo - unaendeleaje? Je, hali ya hewa kule Dar Es Salaam ikoje sasa hivi? Karibu sana uniulize maswali hata kumi na mbili kumi na tatu yahusianayo na Kiingereza! Nitafurahi kuweza kusaidia kuimarisha Wikipedia ya Kiswahili. Uliza tu maswali mengi! Na asante - nimeelewa sasa kwamba ujumbe wengi ni jumbe. Lloffiwr 18:58, 4 Rhagfyr 2008 (UTC)
- Mzee wangu, salam! Mimi sijambo na ninaendelea vizuri tu! Hali ya hewa ya Dar es Salaam, si mbaya. Kuhusu maswali tegemea kero isiyo nakifani, lakini naona mara nyingi una chelewa kujibu ujumbe, je, uko na kazi nyingi sana au huna kawaida ya kufungua hii miradi huria ya Wiki mara kwa mara? Kwa upande nilichelewa kukujibu kwa sababu huwa sina kawaida ya kushriki sana katika mradi huu wa BetaWiki, isipokuwa katika Wikipedia kwa Kiswahili tu, basi. Nikija hapa nakuwa kama mgeni hivyo ukituma ujumbe unaweza ukachelewa kujibiwa kwa kufuatia kutokuwa na watu wanaonisababishia kuwa hapa! Maadam nina wewe, basi nitashiriki mara kwa mara! Awali nilikuwa naogopa kutafsri maneno mengine kwa vile sijui hali ya lugha huko kwenu kwa sasa wanaitaje, yaani kama jinsi unavyoona Kiswahili kila siku kinakuja kipya (sijui kuhusu Kiingereza kama kipo hivyo), na ndiyomaana naogopa kutasfiri zile special:magic! Basi mie sina mengi, we ukiona upo tayari kwa kutafsiri basi tuonane kisha tutaweka mambo sawa, ubarikiwe!!--Muddyb Blast Producer 07:14, 5 December 2008 (UTC)
Muddyb Blast Producer, Salaam. Kuhusu maneno ya kiswahili ya Special pages pamoja na Namespaces nadhani kwamba umefanikiwa kuweka hizi kwa njia ya Special:Magic. Naona kwamba Siebrand aliziweka mpya tarehe 4 mwezi wa kumi na mbili. Ila hujaridhika na picha na faili? Ilipoanza Wikipedia waliita namespace hii IMAGE, yaani picha kwa sababu namespace hii ilikuwa ina tunza picha za Wikipedia. Baadaye wakaongeza uwezo wa kuweka mafaili ya kompiwta ya sauti pamoja na video kwenye namespace ile ile ya IMAGE. Kwa hiyo wamebadilisha jina la namespace iwe FILE. Maana ya Media inapotumika na mafundi wa kompiwta ni haya faili za kompiwta za picha, sauti au video. Maana ya kawaida ya neno la media siku hizi ni 'namna ya kuwasiliana na watu wengi' na hasa kwa njia za gazeti, redio, televisheni, filamu, na kadhalika. Sijui kama hii inakusaidia? Ikiwa unaweka kitu kipya kwenye Special:Magic inabidi uweke ujumbe kwenye Support ili wajue kwamba kuna haja ya kubadilisha faili ya Kiswahili. Na sijui kama umeridhika na kuwekwa kwa majadiliano baada ya Jamii_majadiliano, Msaada_majadiliano, na kadhalika? Naona kwamba ilewekwa sawa kwenye Majadiliano_ya_mtumiaji.
Kuhusu maneno mapya - nakubali kwamba kuna maneno mapya mengi inayoonekana kwenye Kiingereza kila siku, hasa maneno yanayohusika na mambo ya kompiwta na Wikipedia. Ni ngumu mara nyingine kuelewa maana yao wakati maelezo yao yanaandikwa na mafundi wa kompiwta ambao siwaelewi! Kwa kweli kuelewa maana ya jumbe za Mediawiki ndiyo kazi ngumu kuliko kuyatafsiri! Kutunga maneno mapya ya Kiswahili kila wakati pia ni shida - ndiyo sababu mnatoa matoleo mapya ya kamusi pale Tanzania na Kenya na mmeshakuwa mafundi wa kutunga maneno mapya! Kwetu Welisi tunapata shida hiyo hiyo ya kutunga kila wakati. Wakati wa kutafsiri jumbe hizi pamoja na kuandika makala ya Wikipedia tunajaribu kutotunga maneno wenyewe kama yameshatungwa kwenye kamusi fulani au mahali pengine. Lakini mara nyingine hamna kwa hiyo inabidi tutunge wenyewe. Wakati wa kutunga kwa ajili ya jumbe, huwa ninatoa mapendekezo kwenye ukarasa wetu wa majadiliano ya mambo ya lugha [1] - kwenu mnatumia [2] kuzungumza jambo lolote nadhani? Wakati wa kutunga maneno mapya ya Kiwelisi kwenye makala tunaingiza kigezo mwishoni mwa makala ambao inajulisha kwamba kuna maneno mapya yametungwa kwenye makala, inaorodhesha maneno mapya na Kiingereza yao, na pia inaweka makala kwenye jamii ya 'kurasa zinazo maneno yaliyotungwa mapya'. Watu wengine wanapata nafasi ya kutazama maneno mapya. Neno ikipatikana kwenye kamusi fulani au kama baadaye, neno lingine linatungwa nje ya Wikipedia, basi, neno la Wikipedia inaweza kufutwa na lingine kuwekwa badala yake. Tunao pia nia ya kuorodhesha majina haya mapya yote kwenye ukarasa ya pekee ya 'maneno yaliyotungwa kwenye Wicipedia' ila hatujafanya bado - kuna mambo mengi ya kufanya!
Labda ingekuwa afadhali kuzungumza mambo mengine kwenye ukarasa wa Portal_talk:sw au kwenye sw/Wikipedia ili wengine wapate nafasi ya kujadiliana. Unaonaje?
Kuhusu Special/Magic Words - baadhi ya hao yanatumikwa hasa kwenye jumbe za Mediawiki. Sidhani kwamba kuna haraka ya kutafsiri haya. Lakini kuna zingine zinazotumika na watumiaji kwenye kuandika makala:
- #REDIRECT
- magic words zinazo _ pembeni, kwa mfano _NOEDITSECTION_
- magic words zilizoandikwa na herufi ndogo, kwa mfano 'right' 'left'
Maelezo ya maneno haya yanapatikana hapa. Ukitaka kutafsiri maneno haya nipo tayari kusaidia. Baada ya kuyatafsiri katiaka Kiwelisi ikabidi pia nitafsiri ukarasa ya maelezo yao na kuiweka kwenye kurasa za msaada kule Wicipedia ya Kiwelisi. Nimeandika mengi kiasi - nipumzike kiasi - naona kwamba ni saa sita usiku kwenu! Lloffiwr 21:11, 13 December 2008 (UTC)
- Mzee wangu, salam! Wazo la majadiliano yahamie katika Portal sw ni wazo zuri. Au hata kule Uswahilini ni bora zaidi! Kuhusu kutafsiri Special Magic Words, yaani, left, right, redirect, na kadhalika. Hilo mzee wangu we fanya tu! Kwani mie mara nyingi nikifanya huwa nagonga mwamba kwa kufuatia umaskini wa ujuaji wa Kiingereza! Kwa upande wako, ni rahisi mno kufanya hivyo kuliko mie. Kuhusu special pages, hizo nazo naomba uendelee kuzitafsiri, kwani nazo ni tata mno kwangu kwa kufuatia maelezo yako ya juu yahusianayo na mafundi wa software namna wanavyotaja majina ya software kwa namna yao! Lakini bado kwako ni rahisi kufanya hivyo kwa kuwa wewe ndiyo Mwingereza mwenyewe, vipi mimi Mswahili? Hapa naona ndoto za ajabu zikiwa zimeambatana na upepo mkali wa Katrina!! Basi tuendelee kushauriana kwa kila hatua tutakayoipiga katika mijadala yetu!
Kazi njema na tuendeleze lugha zetu. Kwaheri.--Muddyb Blast Producer 09:09, 15 December 2008 (UTC)
- Nikipata nafasi, nitaweka mapendekezo ya kutafsiri Magic Words pamoja na Jumbe kwenye ukarasa wa majadiliano kule wiki ya Kiswahili. Mazungumzo ya juu yamehamishwa hadi hapa toka ukarasa wa User_talk ya Lloffiwr. Lloffiwr 21:15, 12 January 2009 (UTC)
Chumba cha JAMII au CATEGORY
Salaam! Kwa sasa ninatafsiri eneo la JAMII ambalo mara nyingi lilitelekezwa. Je, ungependa kutoa mawazo yako kuhusiana na chumba hii? Naomba fungua hapa ili uweze kuona baadhi ya mabadiliko niliyoyafanya! Kuhusu mjadala wa JAMII hizi, naomba nenda kule Uswalini katika chumba hiki utaona mjadala kuhusu jamii hizi. Ahsante.--Muddyb Blast Producer 06:46, 16 December 2008 (UTC)
- Nimeweka 'wiki link' kwenye Categorytree-desc (“
Dynamically navigate the [[Special:CategoryTree|category structure]]
”). - Categorytree-category (“
Category:
”) ina alama ":" baada yake kwenye Kiingereza. Inaonekana mbele ya sanduku (tazama hapa. Je, huwa inatumikwa alama hii ya ":" kwenye Kiswahili? Lloffiwr 22:21, 12 January 2009 (UTC)
- Mapendekezo nyingine
- no subcategories
- jamii ndogo zake hakuna
- no parent categories
- jamii kuu hakuna
- categories only
- jamii tu
- pages except files
- kurasa isipokuwa mafaili
- no pages or subcategories
- hakuna kurasa wala jamii ndogo zake
- Category $1 not found ($1 ni jina la jamii inayotafutwa)
- Jamii inayoitwa $1 haikupatikana
Lloffiwr 22:35, 12 January 2009 (UTC)
- Mimi zote ninaziona ziko sawa tu, wala sijaona tatizo. Ni vyema hizo jumkbe ngumu zikiwa zinatafsiriwa na wewe! Basi tusonge, kwani kazi bado ndefu!--Muddyb Blast Producer 08:45, 19 January 2009 (UTC)
- Nimeweka zote ila nina wasiwasi kuhusu ile ya mwisho. Nadhani ya kwamba 'Jamii inayoitwa $1 haikupatikana' ndiyo sahihi (si haikupatikana)? Unaonaje? Lloffiwr 13:57, 19 January 2009 (UTC)
- Ndiyo. "Haikupatikana" ni sahihi zaidi!--Muddyb Blast Producer 12:58, 22 January 2009 (UTC)
Mapendekezo mengine ya jumbe
Je, Kiswahili ni sahihi na kinaeleweka?
- Tog-editwidth (“
Widen the edit box to fill the entire screen
”)- Sanduku la kuhariri liwe na upana mzima
- Tog-previewonfirst (“
Show preview when starting to edit
”)- Onyesha mandhari unapoanza kuhariri
- Previousdiff (“
← Older edit
”) - Older edit- Badilisho lililopita
- Nextdiff (“
Newer edit →
”) - Newer edit- Badilisho lijalo
Lloffiwr 19:28, 9 February 2009 (UTC)
- Bado shaka hakuna endapo utatoa wazo lako unaloona sahihi zaidi. Haya ni mambo ya kushirikiana. Hivyo sio rahisi kufanya mtu mmoja halafu iwe sahihi. Fanya masahihisho unayoona ni safi kwa watakaosoma Kiswahili! Sahihisha halafu tuone. Kazi njema.--Muddyb Blast Producer 15:17, 10 February 2009 (UTC)
- Sawa. Je, ipi bora zaidi - neno la siri, au nyiwila? Lloffiwr 23:15, 11 February 2009 (UTC)
- Kwa kweli, sijui kama kuna idadi kubwa ya Waswahili? Ama wanaojua Kiswahili kwa matumizi ya neno la siri kwa jina la "nywila." Naona tuweke "neno la siri" ni bora zaidi kuliko kuwasumbua watu. Au waonaje?--Muddyb Blast Producer 12:59, 21 February 2009 (UTC)
Maswali ya kutafsiri
Je, istilahi gani ni nzuri?
- Print - Chapa, chapisha (chapisha)
- recently - (ya hivi karibuni=ndiyo) (sasa iko 'ya mwisho' kwenye Recentchangeslinked-summary (“
Enter a page name to see changes on pages linked to or from that page. (To see members of a category, enter {{ns:category}}:Name of category). Changes to pages on [[Special:Watchlist|your Watchlist]] are in <strong>bold</strong>.
”)) - Advanced search (Tafuta (kwa-ya?) hali ya juu?)
- With suggestions - na mapendekezo = ndiyo
- No suggestions - bila mapendedezo = ndiyo
- text - maandiko, maandishi = ndiyo, matini (Tooltip-diff (“
Show which changes you made to the text
”))
Lloffiwr 12:25, 21 February 2009 (UTC)
- Nimeonelea hivyo ni sawa, sijui wewe waonaje?--Muddyb Blast Producer 12:48, 21 February 2009 (UTC)
Asante. Tayari. Lloffiwr 20:13, 21 February 2009 (UTC)
Maswali mengine sasa:
- Search results - matokeo ya utafutaji
- Search the pages for this text - 'chunguza kurasa upate maandishi haya', au (=ndiyo: 'tafuta kurasa kwa maandishi haya'.)
- newer - ya karibu zaidi=ndiyo
- older - ya zamani zaidi=ndiyo
- Notitlematches (“
No page title matches
”) - No page title matches - Hakuna jina kama hilo? Rahisi zaidi (sijui kwako?) Jina hili la ukurasa halikupatikana - Anontalk (“
Talk
”) – Talk for this IP - Majadiliano ya IP hii - Ipblocklist (“
Blocked users
”) – Blocked IP addresses and usernames - Anwani za IP na majina ya watumiaji walizozuiwa/waliozuiliwa=ndiyo
Haya, una wazo gani?--Muddyb Blast Producer 16:22, 27 February 2009 (UTC)
- Asante sana - yale yanayotangulia nitayatafsiri. Inabaki mbili ambazo ni vigumu zaidi. Nitayaweka tena kule Wikipedia ya Kiswahili. Lloffiwr 11:45, 28 February 2009 (UTC)
- Namespace - sasa hivi ni ('eneo la majina=ndiyo' -) Special:AllPages. Sijui kama 'eneo' tu ingefaa?
- Nina wasiwasi na hilo 'eneo la majina'. Mifano ya 'namespace' ni - 'kuu', 'mtumiaji', 'majadiliano ya mtumiaji', 'jamii'. Yaani, kuna eneo kuu, eneo la watumiaji, eneo la majadiliano ya watumiaji, eneo la jamii, na kadhalika. Sasa, nikisoma 'eneo la majina' najiuliza - huu ni eneo gani? Ndiyo sababu napendekeza kubadilisha 'eneo la majina' liwe 'eneo' tu. Lakini sijui kama 'eneo' tu lingeeleweka. Labda 'eneo la wiki' lingeeleweka zaidi? Lloffiwr
- Content pages - hizi ni makala kwenye Wikipedia, au mafaili kwenye Wikimedia Commons; yaani, ni kurasa zile za aina ya wiki. Naona labda tukisema (kurasa zilizopo au makala zilizopo inakuwa inaleta maana zaidi?).
- Hata kwenye Kiingereza jina hili halieleweki kirahisi. Napata shida sana ya kupata jina zuri Kiwelisi pia! Wanatumia jina hili kule Wikimedia wakati wanataka kutofautishana kati ya kurasa ambazo ni sehemu ya nia ya wiki (content pages), na kurasa nyingine kama kurasa ya majadiliano, kurasa ya jamii, na kurasa nyingine ambazo ni za kusaidia katika kujenga kurasa za 'content pages'. 'Content pages' huwa zipo ndani ya 'namespace' 'kuu' au 'namespace' mafaili. Una mawazo mengine? Lloffiwr
- Hata mimi nashindwa kutoa wazo lingine kwa sababu nimeelewa vingine kuhusina na neno hili. Basi tafuta jina ambalo unahisi litafaa kulitumia kuita CONTENT PAGES! Halafu ninaswali moja: Unataka kuniambia Wawelisi hawajui Kiingereza? Na kama wanajua, kuna ulazima gani wa Wawelisi kuwa na Wikipedia yao ilhali Kiingereza wanakijua? Swali linaonekana kutokuwa na msingi wowote, lakini ningependa kujua! Kila la kheri.--Muddyb Blast Producer 12:00, 3 March 2009 (UTC)
Maswali mawili haya yamepelekwa Wikipedia ya Kiswahili.
Je, ipi kati ya hizi mbili ni Kiswahili sanifu?
- MediaWiki:Lastmodifiedat/sw Ukarasa huu umebadilisha mara iliyopita tarehe $1, saa $2.
- MediaWiki:Lastmodifiedatby/sw Ukurasa huu ulibadilishwa mwishoni saa $2, tarehe $1 na $3.
Ujumbe mmoja wao unaonekana mwisho wa kila ukurasa. Lloffiwr 18:17, 7 March 2009 (UTC)
kutafsiri 'section'
'section' imetafsiriwa 'fungu', 'sehemu' na 'kipande' kwenye jumbe mbalimbali. Je, ipi ni bora? Lloffiwr 21:29, 3 April 2009 (UTC)
jumbe za copyright
inafuata jaribio la tafsiri ya Copyright (“-
”). Nimetoa links kwa sasa hivi ili ieleweke kirahisi.
Kiingereza: Text is available under the Creative Commons Attribution/Share-Alike License; additional terms may apply. See Terms of Use for details.
Kiswahili: Maandishi inapatikana yanapatikana chini ya leseni ya Creative Commons Attribution/Share-Alike License; matakwa mengine yanaweza kutakiwa.
Tazama maelezo zaidi ya Matakwa ya Utumiaji.
Je, tusitafsiri Creative Commons Attibution/Share-Alike kwa sasa? Lloffiwr 10:51, 4 July 2009 (UTC)
Sidhani kama kuna ulazima wa kutafsiri jina la leseni/hatimiliki.. Labda tungeacha kama inavyojieleza!--Muddyb Blast Producer 10:58, 4 July 2009 (UTC)
Imesahihishwa Lloffiwr 11:21, 4 July 2009 (UTC)
- Inafuata jaribio la tafsiri ya Copyrightwarning (“
Please note that all contributions to {{SITENAME}} are considered to be released under the $2 (see $1 for details). If you do not want your writing to be edited mercilessly and redistributed at will, then do not submit it here.<br /> You are also promising us that you wrote this yourself, or copied it from a public domain or similar free resource. <strong>Do not submit copyrighted work without permission!</strong>
”). Nimetoa links kwa sasa hivi ili ieleweke kirahisi.
Kiingereza: By saving, you agree to irrevocably release your contribution under the Creative Commons Attribution/Share-Alike License 3.0 and the GFDL. You agree to be credited by re-users, at minimum, through a hyperlink or URL to the page you are contributing to. See the Terms of Use for details.
Kiswahili: Unapohifadhi maandishi yako, unakubali (kwa jinsi isiotenguka) mchango wako utolewe chini ya leseni za (ya/sio za) Creative Commons Attribution/Share-Alike License 3.0 pamoja na GFDL.
Unakubali utambuliwe wakati maandishi haya yatumika na wengine, angalau kwa nia ya kiungo (hyperlink) au URL kwenye ukurasa uliouchangia.
Tazama maelezo zaidi ya Matakwa ya Utumiaji.
- Inafuata jaribio la tafsiri ya Editpage-tos-summary (“
-
”). Nimetoa links kwa sasa hivi ili ieleweke kirahisi.
- Inafuata jaribio la tafsiri ya Editpage-tos-summary (“
Kiingereza: If you do not want your writing to be edited and redistributed at will, then do not submit it here. If you did not write this yourself, it must be available under terms consistent with the Terms of Use, and you agree to follow any relevant licensing requirements.
Kiswahili: Ikiwa usingependa maandashi yako yabadilishwe au yatumike mahali pengine na wengine, usichangie hapa. Ikiwa hukuandika mchango huu mwenyewe, lazima upatikane chini ya matakwa yanayolingana na Matakwa ya Utumiaji yanayotumika hapa, na unakubali kufuata matakwa yeyote ya leseni yake.
jumbe za pili na tatu. Lloffiwr 12:02, 4 July 2009 (UTC)
TAZAMA HII:
Ikiwa hutaki maandashi yako yahaririwe na yatumike kwa hiari, basi usiyaweke hapa.
Kidogo kama ni afadhali?--Muddyb Blast Producer 12:14, 4 July 2009 (UTC)
Sawa. nitayaweka. Lloffiwr 13:00, 4 July 2009 (UTC)